Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Date
2023-09-11Author
Melly, Joachim Kipchirchir
Mohochi, Ernest Sangai
Metadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika kuwasilisha maudhui ya kidini, sera za matumizi ya lugha, na athari ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika kuwasilisha ujumbe wa kidini. Nadharia ya umilisi mawasiliano yake Dell Hymes (1966) iliongoza utafiti. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji, mahojiano na uchunzaji. Wanafunzi thelathini wa kidato cha nne, viongozi kumi wa kidini wa wanafunzi na kasisi mmoja wa shule walihusishwa katika ukusanyaji wa data. Matokeo yalibaini kuwa sera ya lugha katika shule ya wasichana ya Itigo ilipendelea matumizi ya Kingereza kama lugha ya mawasiliano. Wanafunzi walisema kuwa lugha ya Kiswahili inapotumika katika mahubiri, ujumbe hueleweka zaidi. Vilevile, ilidhihirika kuwa viongozi wa kidini wa wanafunzi hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana katika mikutano yao lakini wao huandika kumbukumbu kwa lugha ya Kiingereza. Isitoshe, ilibainika kuwa lugha anayoitumia zaidi kasisi wa shule katika mahubiri yake ni Kiingereza. Licha ya uwezo wa Kiswahili katika kufanikisha mawasiliano kuhusu maswala ya kidini shuleni, Kiingereza ndicho hutumika zaidi. Kunahitajika mabadiliko katika sera ya lugha shuleni ili kuipa lugha ya Kiswahili nafasi zaidi katika mawasiliano ya kidini.