Show simple item record

dc.contributor.authorSangili, Nabeta Nixon Kenyani
dc.date.accessioned2023-03-24T11:26:48Z
dc.date.available2023-03-24T11:26:48Z
dc.date.issued2019-11
dc.identifier.urihttp://repository.rongovarsity.ac.ke/handle/123456789/2494
dc.description.abstractTafiti nyingi zimefanywa katika lugha mbalimbali hapa nchini Kenya na ulimwengu mzima kuhusu kutoweka kwa lugha kwa sababu ya kutodumishwa. Tatizo hili limetambuliwa na madola ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika mbali na mataifa binafsi mbalimbali. Baadhi ya lugha zilizotafitiwa awali, kupitia kwa wasemaji wake, zilihama maaeneo yake asilia na kuhamia kwingineko. Kimaragoli kinachozungumzwa katika eneobunge la Uriri ni mojawapo ya lugha zilizohamia maeneo tofauti na maeneo yake. Suala ni kwamba, japo tafiti zimefanywa kwingineko, panahitaji tafiti zaidi kuhusiana na hali ya Kimaragoli katika eneobunge la Uriri. Utafiti huu ulitambua pengo hili na kudhamiria kutafitia udumishaji wa Kimaragoli katika eneo Uriri. Ili kutimiza lengo hili, utafiti huu uliongozwa na madhumuni yafuatayo : kuchunguza mikakati inayotumika kudumisha lugha ya Kimaragoli katika eneobunge la Uriri ; kutathmini umilisi wa lugha ya Kimaragoli miongoni mwa wasemaji wake katika eneobunge la Uriri ; kubainisha athari ya lugha ya Kiluo katika Kimaragoli na kujadili mielekeo ya wasemaji wa Kimaragoli na Kiluo kuhusu uzungumzaji wa lugha ya Kimaragoli katika eneobunge la Uriri. Nadharia za Mtagusano Lugha iliyoasisiwa na Weinreich (1953) na kuboreshwa na Thomason na Kauffman (1988) na Uzalishaji Kijamii iliyoasisiwa na Bourdieu (1977) na Uhuishaji Kiethnoisimu ya Giles, Bourhis na Taylor (1977) zilikuwa kiunzi cha utafiti huu. Utafiti huu ulitumia miundo ya Uauzi na Uchanganuzi Linganishi. Idadi jumla ya watafitiwa ilikuwa Wamaragoli 20,000 katika Wadi 5 za eneobunge la Uriri. Fomula ya Yamane (1967) ilitumika kupata sampuli wakilishi ya watafitiwa 390 walioteuliwa kimaksudi. Mbinu ya kupata sampuli ya kimaksudi pia ilitumika kupata watafitiwa 5 na wanakundi 10 kwa ajili ya mahojiano na mijadala. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji, mahojiano, mjadala wa kundi lengwa na ratiba ya uchunzaji. Uaminikaji na Udhabiti wa vifaa vya utafiti ulifanyiwa Idarani baada ya Utafiti awali kufanyika. Data ya kiwingiidadi ilichanganuliwa kwa kutumia idadi za kiumaratokezi, asilimia na kuwasilishwa kwa kutumia chati duara, majedwali, grafumihimili na maelezo. Data ya kithamano ilinukuliwa, kutafsiriwa na kusarifiwa kwa kuzingatia maudhui mbalimbali na unukulishi wa data iliyorekodiwa ulifanywa kimaandishi. Matokeo ya utafiti yalionyesha kwamba mikakati inayopendelewa sana ni matumizi ya idhaa za Kimaragoli wastani (75.8%), watoto kufundishwa Kimaragoli na wazazi wastani (73.2%) na kuongoea Kimaragoli nyumbani wastani (72.7%). Aidha, utafiti ulibaini kwamba wazee na makamo wana kiwango cha juu cha umilisi wa kimsingi wa Kimaragoli (93.4%), ikifuatiwa na watoto (93.3%) na vijana (89%). Umilisi huu kwa vijana na watoto unaathiriwa na utangamano na Kiluo. Utafiti ulitambua kwamba Kimaragoli kimeathiriwa pakubwa na Kiluo katika maeneotumizi, kileksimu na pia kwa wasemaji wa Kimaragoli. Uchanganyaji na uhamishaji ndimi kati ya Kimaragoli na Kiluo unashuhudiwa sana miongoni mwa vijana na watoto. Pia, utafiti huu ulitambua kwamba Wamaragoli wana mielekeo chanya kuhusu lugha yao ijapokuwa inatofautiana kiumri. Hata hivyo, mwelekeo ulikuwa wastani wa 83.4%. Matokeo haya yanaashiria kwamba Kimaragoli kinadumishwa kutokana na mikakati imara, umilisi wa kiwango cha juu, kutoathiriwa pakubwa kileksimu na kuwepo kwa mwelekeo chanya miongoni mwa Wamaragoli na Waluo. Matokeo haya yatakuwa amilifu kwa wataalamu wa kupanga lugha katika jamii, taaluma ya Kiswahili katika kujenga dafina ya mtagusano isimu, Wizara ya Elimu na dola za Kimataifa hasa AU na UNESCO wanaohusika katika utafiti wa kuhatarishwa kwa Lugha na Mikakati ya Uhuishaji wa Lugha ulimwenguni kote.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.subjectUchumi, Jamii Isimu .en_US
dc.titleUdumishaji wa lugha ya kimaragoli katika eneobunge la Uriri, Kenyaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record