Lugha na utambulisho: tofauti katika matumizi ya kiswahili nchini tanzania na Kenya
Abstract
Matumizi ya lugha moja hutofautiana kwa kutegemea mambo kama vile umri, jinsia, tabaka na
maeneo ya kijiografia miongoni mwa mengine. Matokeo ya hali ni kuwa matumizi ya lugha
huishia kutoa mchango mkubwa katika utambulisho wa watumiaji wake. Makala hii inamulika
hali ya matumizi ya kila siku ya lugha ya Kiswahili nchini Tanzania na Kenya, lengo kuu likiwa
kutambua na kujadili tofauti mbalimbali zinazojitokeza katika matumizi hayo ya lugha. Makala
itatafutia maswali yafuatayo majibu: Ni kwa kiasi gani tofauti katika matumizi hayo ya lugha ya
Kiswahili yanawatambulisha wananchi wa nchi hizo mbili? Tofauti hizo zinaweza kusababisha
matatizo yoyote katika mawasiliano pamoja na maingiliano ya kila siku katika shughuli
mbalimbali? Hali hiyo inaweza kuathiri maendeleo ya kijamii pamoja na ujenzi wa ushirikiano
katika eneo la Afrika Mashariki? Nini chaweza kufanyika ili kuelewesha wahusika kuhusu
matumizi tofauti ya lugha hiyo ili kuhakikisha kuwa hayawi kikwazo katika mawasiliano
miongoni mwa watumiaji wa Kiswahili katika nchi hizo?
Collections
The following license files are associated with this item: