Dhuluma kama kichocheo cha mzinduko wa wanawake katika riwaya ya kiswahili
Abstract
Kwa kipindi kirefu wanawake wametwezwa na kudunishwa kutokana na dhuluma wanazofanyiwa na jamii
inayotawaliwa na mfumo wa kuumeni. Dhuluma wanazopata wanawake zinatokana na asasi tofauti tofauti
ambazo ndizo zinapaswa kudumisha mshikamano wa kijamii. Tahakiki na tafiti nyingi zinaonyesha athari ya
ukandamizaji wa jinsia ya kike na hali ya kuzimwa kwa juhudi zake katika kupigania nafasi yake. Mwanamke
anavyoitikia hali hii kwa njia inayomzindua na kumfaidi ni suala ambalo halijaangaziwa pakubwa. Ni
kutokana na msingi huu ambapo makala hii inachunguza namna dhuluma wanazopata wanawake
zinavyowazindua na kuwapa motisha ya kujikomboa na kujinasua kutokana na hali hii ya kusakamwa na asasi
kandamizi za kijamii. Kwa njia hii, wanawake wanapata nafasi ya kujiendeleza katika nyanja mbalimbali
ikiwemo kujieleza kimapenzi badala ya kuridhia kuishi vivulini mwa waume zao dhalimu. Hali hii inampa
mwanamke taswira mpya kama kiumbe mwenye thamani na mchango mkubwa katika kuongoza juhudi za
ufanisi wa jamii yake. Uchunguzi huu umeegemea fasihi andishi ya Kiafrika kwa kurejelea kazi mbili: Nyuso
za Mwanamke (Mohamed, 2010) na Heri Subira (Babu, 2010). Riwaya hizi ziliteuliwa kwa kutumia mbinu ya
uteuzi wa kimakusudi. Riwaya hizi zimesheheni hali ngumu ya maisha wanayopitia wahusika wa kike hasa
katika harakati zao za kujinasua kiuchumi na kujisaka kimapenzi. Aidha zimeangazia masuala ya wanawake
kwa uangavu na kwa namna inayopanua nafasi ya jinsia ya kike katika dunia ya kisasa. Kutokana na mchango
mkubwa wa wanawake katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa jamii, ni bayana kuwa matumizi ya fasihi
Collections
- School of Education [137]