Lugha na utambulisho: tofauti katika matumizi ya kiswahili nchini tanzania na Kenya

Loading...
Thumbnail Image

Date

2015

Authors

Mohochi, Sangai

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chama cha Kiswahili Africa Mashariki (CHAKAMA)

Abstract

Matumizi ya lugha moja hutofautiana kwa kutegemea mambo kama vile umri, jinsia, tabaka na maeneo ya kijiografia miongoni mwa mengine. Matokeo ya hali ni kuwa matumizi ya lugha huishia kutoa mchango mkubwa katika utambulisho wa watumiaji wake. Makala hii inamulika hali ya matumizi ya kila siku ya lugha ya Kiswahili nchini Tanzania na Kenya, lengo kuu likiwa kutambua na kujadili tofauti mbalimbali zinazojitokeza katika matumizi hayo ya lugha. Makala itatafutia maswali yafuatayo majibu: Ni kwa kiasi gani tofauti katika matumizi hayo ya lugha ya Kiswahili yanawatambulisha wananchi wa nchi hizo mbili? Tofauti hizo zinaweza kusababisha matatizo yoyote katika mawasiliano pamoja na maingiliano ya kila siku katika shughuli mbalimbali? Hali hiyo inaweza kuathiri maendeleo ya kijamii pamoja na ujenzi wa ushirikiano katika eneo la Afrika Mashariki? Nini chaweza kufanyika ili kuelewesha wahusika kuhusu matumizi tofauti ya lugha hiyo ili kuhakikisha kuwa hayawi kikwazo katika mawasiliano miongoni mwa watumiaji wa Kiswahili katika nchi hizo?

Description

Keywords

Citation