Mabadiliko ya Itikadi za Ujinaishaji katika Jamii ya Wakuria

dc.contributor.authorMwikali, Roseline
dc.contributor.authorMohochi, Ernest
dc.contributor.authorOgola, James
dc.contributor.authorOlal, Francis Ongachi
dc.date.accessioned2024-12-09T10:13:29Z
dc.date.available2024-12-09T10:13:29Z
dc.date.issued2024-11-27
dc.description.abstractDunia ya leo ya kiutandawazi inawezesha mtagusano wa umma wa kimataifa kidijitali unaoendelea kushuhudia utamaduni chipukizi wa ujinaishaji unaozidi kushika kasi. Hivyo, makala hii inachanganua mabadiliko katika ruwaza za ujinaishaji yanayotokana na athariya elimu ya magharibi, dini, teknolojia, na utawala katika jamii ya Wakuria pamoja na athari zake. Wakuria ni jamii ndogo ya kundi la Wabantu wa Magharibi inayopatikana katika Kaunti ya Migori nchini Kenya kwenye ujirani na nchi ya Tanzania. Ujinaishaji ni sehemu muhimu ya maisha ya jamii ya Wakuria kwani ni utambulisho wao. Aidha, sawa na jamii nyingine zile, ujinaishaji huwa dafina ya historia yao. Nadharia ya Uchanganuzi Hakiki wa Usemi mtazamo wa Kihistoria yao Wodak na Reisgil(2001)ilikuwadira katika uchanganuzi wa data zilizokusanywa. Data ambayo imetumika katika makala hii ilikusanywa kwa njia ya mahojiano ya ana kwa ana pamoja na majadiliano ya makundi. Idadi ya sampuli ilikuwa watu 42; wa kike 18 na wa kiume 24. Makala hii imebainisha kuwa mabadiliko ya kielimu, kiuchumi, kiteknolojia, kiutawala na kidini yamekuwa na athari kubwa kiitikadi katika ujinaishaji miongoni mwa Wakuria. Majilio ya elimu ya magharibi, uhuru wa kufanya biashara, mifumo ya kisiasa na mtagusano wa kiteknolojia umepelekea ukopaji wa majina kutoka makabila mengine nchini Kenya na ulimwenguni kote miongoni mwa jamii ya Wakuria. Hili linamaanisha kuwa itikadi za ujinsia zilizohodhiwa na kushamirishwa na majina ya kiasili ya Wakuria zinazidi kufifia kila uchaoen_US
dc.identifier.citationRoseline M., Ernest M., & James O. (2024). Mabadiliko ya Itikadi za Ujinaishaji katika Jamii ya Wakuria. Jarida la Kiswahili Sanifu 1 (2024), 18–25.en_US
dc.identifier.urihttp://repository.rongovarsity.ac.ke/handle/123456789/2726
dc.language.isoswen_US
dc.publisherJarida la Kiswahili Sanifuen_US
dc.relation.ispartofseriesVol. 1;No. 003
dc.subjectUjinaishaji, Itikadi, Nadharia,Wakuria,en_US
dc.titleMabadiliko ya Itikadi za Ujinaishaji katika Jamii ya Wakuriaen_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
jakisa0003.pdf
Size:
406.17 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: